Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wafanyikazi wa umma kwenye serikali ya Kaunti ya Nyamira waonywa dhidi ya utoaji wa huduma duni kwa wananchi.

Gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama, aliyekuwa akizungumza katika eneo la Tinga siku ya Alhamisi, alisema kuwa sharti wafanyikazi wa umma wawajibike kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi. 

"Sharti wafanyikazi wa umma wawajibike kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi na ninawaomba wananchi kuwaripoti maafisa wasio wajibika kazini,” alisema Nyagarama.

Gavana Nyagarama alisema ni jambo la kushangaza kwamba kuna baadhi ya wafanyikazi waliomo maafisini, ilhali hawatoi huduma zinazo tarajiwa kutoka kwao.

"Kuna baadhi ya wafanyikazi waliomo maafisini bila kutoa huduma wananchi wanazo zitarajia kutoka kwao. Ninawaonya kwamba serikali yangu haitasita kuwachukulia hatua maafisa hao,” alisema Nyagarama.

Akizungumzia swala lakuimarisha sekta ya kilimo kwenye Kaunti ya Nyamira, Gavana Nyagarama alisema kuwa serikali yake imeweka mikakati yakustawisha kilimo kwa kuwa kilimo huchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi.

"Serikali yangu imeweka mikakati kabambe yakuhakikisha kuwa ukuaji wa kilimo unaimarika hata zaidi kwa kuwa kilimo huchangia pakubwa kwenye ukuaji wa uchumi nchini,” alisema Nyagarama.