Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanasiasa kutoka eneo bunge la Kitutu Masaba, Kaunti ya Nyamira, Victor Swanya, amewaomba wahisani kujitokeza kusaidia mayatima kutoka eneo bunge hilo ili kujiendeleza kimasomo.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa kuna mayatima wengi katika eneo bunge hilo ambao wanahitaji msaada ili kujiendeleza kimasomo.

Kulingana na mwanasiasa huyo, kuna haja ya wale wamefanikiwa katika maisha yao kujitolea kutoa msaada kwa Jamii.

Akizungumza siku ya Alhamisi huko Kitutu Masaba, Swanya aliwaomba wahisani kujitokeza kutoa msaada kwa mayatima.

“Wengi wa mayatima katika eneo hili wako na nia ya kusoma lakini hawana uwezo wa kugharamia masomo hayo,” alisema Swanya.

Aliongeza, “Naomba tujiunge pamoja ili tutoe msaada kwa watoto mayatima ili nao waje kusaidia jamii katika siku za usoni.”

Swanya pia aliomba serikali ya kaunti hiyo kuingilia kati na kuwasomesha wanafunzi hao.