Wakaazi wa eneo bunge la Bomachoge Borabu na Bomache Chache kaunti ya Kisii wamekubaliana kufanya maendeleo pamoja ili eneo hilo la Bomachoge liinuke zaidi.
Akizungumza siku ja Jumamosi katika eneo la Mogonga eneo lililoko Bomachoge Borabu kwa hafla ambayo iliandaliwa na chama cha wakaazi hao, wakili Edward Begi alisema wakaazi wa maeneo bunge hayo mawili wamekubaliana kufanya kazi pamoja jinsi ilivyokuwa hapo mbeleni
Maeneo bunge hayo mawili yalikuwa katika eneo bunge moja ambalo lilikuwa likiitwa Bomachoge, lakini bunge hilo likagawanywa na kuwa maeneo bunge mawili; Bomachoge Chache na Bomachoge Borabu, jambo ambalo limefanya maendeleo kurudi nyuma zaidi.
“Tutaendelea kukutana wakaazi wa maeneo bunge haya mawili na kupanga yale maendeleo tunataka yafanywe hapa Bomachoge,” alisema Begi.
Wakaazi hao wameomba viongonzi wote wa maeneo hayo kuanzia wawakilishi wa wadi za eneo hilo pamoja na wabunge kushirikiana na kuweka masuala ya kisiasa kando na kuwatumikia wananchi wa maeneo hayo.
“Sisi lile tunahitaji ni maendeleo na hiyo ndio ombi letu na hata wakati tulichagua viongonzi wao wenyewe walikuwa wakisema ni maendeo yatapewa kipao mbele na sasa tunataka kushuhudia maendeleo hayo yakifanywa,” alihoji Felix Ong’era, mkaazi.