Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa mtaa wa Mwembe ulioko mjini Kisii wamewaomba maafisa wa usalama kuhakikisha wameimarisha usamala katika eneo hilo na kukabiliana na wezi wanaowaibia na kuwaangaisha.

Wakiongea siku ya Jumatano na mwaadishi huyu katika mtaa wa Mwembe, baadhi ya wakazi walisema kuwa kuna watu wanaowangaisha kwa kuwaibia bidhaa mbalimbali kutoka kwa nyumba zao haswa wakati wamo kazini.

Wakaazi hao walisema kuwa wakitoka kazini wakati wa jioni hufika nyumbani na kupata milango ya nyumba zao imevunjwa na baadhi ya vifaa kama runinga na gesi zimeibiwa.

"Tumekuwa tukishuhudia wizi katika mtaa huu kwa muda mrefu huku vitu vikiibiwa na wakora walioko katikati yetu," alisema  Lydia Kwamboka, mkaazi.

Kwa sasa wamewaomba maafisa wa polisi katika kituo kilochoko Mwembe katika ofisi ya chifu wa lokesheni ya Campus kuwajibikia na kuwasaka wezi hao kwani wamechoshwa na vitendo hivyo.

"Naomba maafisa wetu kuwasaka wezi hoa kwani wamekuwa wakitusumbua sana. Mtu hawezi fanya kazi kwa amani kwa kuwa huwa tunafikiria vitu vyetu ambavyo viko nyumbani kama viko sawa au vimeporwa," alisema John Oyaro, mkaazi.