Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa Mochenwa wadi ya Gesima wamemuomba chifu wa lokesheni hiyo kuchukua hatua ya kisheria kwa mgema mmoja ambaye anaendelea kuuza pombe haramu katika eneo hilo.

Wakiongea hii leo, Jumatatu na mwaandishi huyu katika eneo ya Nyabiosi, wakaazi hao walimshtumu chifu wa lakosheni hiyo Magara Makori kwa kutomchukulia hatua mgema huyo ambaye anaendelea kuuza pombe.

Kulingana na wakaazi hao, mgema huyo kwa jina la utani ‘Mama Royco’ amekuwa akiendelea kuuza pombe licha ya serikali kuagiza pombe hiyo kukoma kupikwa kote nchini.

Kwa sasa wakazi hao wamemuomba chifu huyo kukomesha ugemaji huo, au la wataandamana kulalamikia swala hilo.

“Sisi kama wakaazi tumeripoti pombe hiyo kila mara na kwa sasa tunataka hatua ya haraka kuchukuliwa kwani tumechoshwa na mgema huyu,” alihoji Vivian Mong’ina, mkaazi.

Kwingineko, waliomba wanaomwaga pombe katika msako ambao unaendelea kutomwaga pombe hiyo kuelekea mtoni kwani inachafua maji na watu wengi hutegemea maji ya mito katika eneo hilo.

“Tunaomba kuwa wakati pombe inamwagwa isikuwwe inamwagwa kuelekea mtoni kwani pombe hiyo uchafua maji na mazingira, kwa hivyo inahitajika kuwa na mahali pa kumwaga pombe ili kutunza mazingira,” allihoje Susan Nyaribo, mkaazi mwingine.