Wakazi wa kaunti ya Nyamira wameshauriwa kutopanda miti karibu na mito ili kutunza mazingira.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika eneo la Mongori, eneo bunge la Borabu kaunti ya Nyamira wakili Alfaxard Moikoyo aliomba wananchi wa kaunti hiyo kutopanda miti karibu na mito huku akisema insababisha mito kukauka.
Amesema kuwa ni sharti wenyeji waitunze mito ambayo hulinda dhidi ya ukosefu wa maji.
“Naomba kila mtu atunze mazingira maana tukiwa na mazingira mabaya maisha yetu ni duni. Isitoshe, mito ikikauka ukulima utaanza kufifia,”alisema.
“Kulingana na sheria za mazingira hakuna mtu anaruhusiwa kupanda miti karibu na mito maana maji yanaweza kukauka na hiyo ni hasara kwetu haswa kukosa maji,” aliongeza Moikoyo
Wakili huyo alitumia fursa hio kuwaomba vijana wote wa kaunti ya Nyamira kufanya kazi ili kujiendeleza kimaisha kwa ukulima.
Aliwaeleza kuwa kilimo kina faida nyingi kushinda kutegemea ajira za ofisini.