Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakazi wa Wadi ya Keumbu, Kaunti ya Kisii, watanufaika kutokana na mradi maji huku wakionywa kutayotumia kwa muda wa wiki moja hadi yawe masafi kama njia moja ya kujilinda kiafya.

Akiongea siku ya Jumapili katika hafla ya kuchangisha pesa katika kanisa ya Mtakatifu Paulo ya Amasago, mwakilishi wa wadi ya Keumbu, eneo bunge la Nyaribari Masaba, Kennedy Nyakundi, alisema kuwa kila mkazi wa wadi hiyo atapata maji katika boma lake.

Nyakundi alisema kuwa kutokana na mradi wa maji ulioanzishwa na serikali ya kaunti ya Kisii katika shule ya upili ya Amasago kwa kuchimba kisima, sasa kuna uwezo wa kisima hicho kuwasadia wakazi wote.

“Kutokana na kisima kilichochimbwa katika shule yetu ya Amasago, sasa ni furaha kuwa wadi yetu itakuwa na maji na kila mmoja wetu atanufaika na mradi huo ikiwemo hospitali yetu ya keumbu,” alisema Nyakundi.

Aidha, alipongeza serikali ya kaunti kwa mradi huo huku akisema wakazi sasa watapata matunda ya serikali za ugatuzi.

Kwa upande mwingine, aliomba tume ya kuwaajiri walimu pamoja na serikali kuu kusikia kilio cha walimu na kuwalipa mshahara wao ndiposa waweze kurudi shuleni.

“Naomba serikali kusikia kilio cha walimu ili kutusaidia kwa kuwa watoto wetu wanaumia wakiwa nyumbani ilhali ni muhula wa tatu,” aliongezea Nyakundi.