Wakazi wa eneo la Ibecho eneo bunge la Bomachoge Chache, Kaunti ya Kisii wamelalamikia kutengwa na kuachwa nje katika nafasi za ajira katika serikali ya kaunti hiyo.
Kulingana nao, hakuna mtu kutoka eneo hilo aliyechaguliwa kufanya kazi katika serikali ya kaunti ya kisii.
Wakizungumza siku ya Jumatatu wakati wakazi hao walikuwa na mkutano wa kutaka kubaini eneo la Ibecho linapatika katika wilaya ipi, wakazi hao wakiongozwa na Peterson Osante walisema tangu serikali za ugatuzi zianzishwe nchini, hawajawahi nufaika vyovyote kama wakazi wa kaunti ya Kisii hasa kwa nafasi za ajira.
Wakazi hao wameiomba serikali ya kaunti ya Kisii kuonyesha uwazi kwa wakazi wote wa kaunti hiyo na kuwahusisha katika nafasi za ajira pindi zinapotokea kwa kaunti hiyo.
“Mbunge wa eneo bunge hili Simon Ogari anatoka wilayani kenyenya, nainu gavana wa kaunti ya Kisii Maangi anatoka Kenyenya, Mkurugenzi wa kaunti anatoka Kenyenya, mwakilishi mteule anatoka kenyenya, naibu mkurugenzi anatoka kenyenya kwani sisi wakazi wa Ibecho tulizaliwa kupiga kura pekee na kutengwa katika nafasi za ajira,” aliuliza Osante.