Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakulima wa nafaka kutoka Uasin Gishu wameitaka serikali kuhakikisha kuwa wamepokea mashine ya kukausha nafaka mashambani msimu wa El Nino.

Wakizungumza siku ya Jumatano, wakulima hao walisema licha ya serikali kutoa ahadi kwamba wataletewa mashine hiyo mashambani, bado mashine hiyo haijawafikia.

John Kiprop, ambaye ni mkulima wa ngano na mahindi katika eneo la Ilula mjini Eldoret, alisema kwamba wameanza kuvuna nafaka mapema kama tahadhari dhidi ya El Nino.

Bw Kiprop alisema hatua ya serikali kutangaza kwamba kutakuwa na mvua ya El Nino imewafanya kuanza kuvuna mazao yao mapema hivyo basi watahitaji mashine ya kukausha nafaka hiyo.

Mkulima huyo alielezea wasiwasi ya kupata hasara kutokana na mchakato wa kuvuna nafaka mapema.

“Sisi tunahofia kupata hasara kubwa msimu huu kwani nafaka ambayo tunavuna bado ina unyevunyevu,” alisema Kiprop.

Wakulima hao wanataka serikali kuhakikisha kuwa wamepata usaidizi unaostahili kukabiliana na hasara hiyo.

Msimamo wa wakulima hao umeungwa mkono na mtetezi wa wakulima Bi Moira Chepkok, ambaye alitaka serikali kusaidia wakulima kukabiliana na changamoto ya El Nino.

Bi Chepkok alisema kutokana na hofu ya kupata hasara, wakulima wengi wamevuna mazao yao mapema na huenda hawatapata faida inayostahili.

“Msimu huu mavuno ya nafaka imeenda chini sana kwani mahala ambapo sisi huvuna magunia kama 20 ya nafaka tumevuna magunia chini ya 10,” alisema Chepkok.

Chepkok aliitaka serikali kaumrisha kufunguliiwa mapema kwa mabohari ya bodi ya nafaka na mazao nchini ili kuwezesha wakulima kuasillisha mazao yao kwa bodi hiyo kwa wakati unaofaa.