Share news tips with us here at Hivisasa

Wakulima wa majani chai kutoka Kaunti ya Nyamira wameombwa kutunza mimea hizo kuhakikisha mapato mema katika siku zijazo.

Akiongea na wakulima wa majani chai katika kituo cha kununua majani chai cha Riaking’oina katika kijiji cha Matunwa iliyoko Wadi ya Gesima wakati wa kuwapokeza mbolea, Mwenyekiti wa wakulima aliyemwakilisha mkurugenzi, Jackson Atera aliwaomba wakulima wote kutunza mmea huo ili kupata mapato mema katika pesa za ziada za mwaka huu.

Aidha, mwenyekiti Atera alisema kampuni ya majani chai ya Nyansiongo imeweka mikakati ya kuwasaidia wakuliama kukuza mmea huo kama njia moja ya kupata mapato mema kutoka kwa mmea huo.

Atera aliwahimiza wakulima kutumia mbolea hiyo kwa mmea huo akidai kuwa baadhi ya wakulima wa majani chai hao wana tabia ya kutumia mbolea hizo kwa upanzi wa mimea mbadala kinyume na sheria ya kampuni ya KTDA.

“Mnapo pewa mbolea hizi mnastahili kuzitumia kwa mmea wa majani chai ili mmea huo uweze kutoa mazao mema,” aliongezea mwenyekiti Atera.

Kwingineko, wakulima wameombwa kuhudhuria mafunzo yanayotolewa jinsi ya kutunza mmea huo wakati kampuni hiyo inaitisha mkutano wa mafunzo hayo.

Kwa upande wa wakulima hao, waliiomba kampuni hiyo kuwaongeza mbolea na ili kutunza mmea huo ipasavyo.

“Tunaiomba kampuni yetu kutuongeza kiwango cha mbolea ili tuweze kusaidika na mmea huu zaidi,” alihoji Grace Nyagicha, mkulima.