Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Msongamano katika maduka ya mbegu umeshuhudiwa Mombasa wakati huu ambapo msimu wa mvua unatarajiwa.

Katika maduka eneo la soko la Marikiti, wateja wanaonekana kufurika wakinunua mbegu tayari kwa upanzi.

Wakizungumza siku ya Jumapili na mwandishi huyu, wauzaji katika maduka hayo walisema kuwa mauzo ya bidhaa hizo umeshamiri pakubwa hasa tangu mwanzo mwa wiki jana.

Omar Salim, mmoja wa wakulima alisema kuwa huu ni wakati mwafaka wa upanzi huku akiwataka wakulima kutohofia kuwa huenda mvua ikanyesha nyingi kupita kiasi na kuharibu mimea.

“Huu ni wakati mwafaka wa upanzi na nimejitayarisha pakubwa kupanda mahindi na vyakula vyinginevyo,” alisema Omar.

Hata hivyo alidokeza kuwa ni vyema kupanda mimea inayostahamili mvua nyingi hasa katika mashamba yalio sehemenu za chini.