Wakazi wa Kaunti ya Nyamira na Kisii wameombwa kupanda miti ya aina ya Bamboo kama njia moja ya kuzuia mmonyoko wa udongo na kutunza mazingira.
Akiongea na wakulima siku ya Ijumaa katika uwanja wa Gusii katika maonyesho ya kilimo, Meneja Mkuu wa Lake Basin Development Authority (LBDA) Zephania Atieno aliyewaomba wakulima kupanda mti ya aina ya Bamboo, alisema kuwa miti hiyo haina madhara yoyote kwa binadamu na mazingira.
“Nawaomba wakulima wote kupanda miti hii ya bamboo kama njia moja ya kutunza mazingira yetu,! alihoji Atieno.
Meneja huyo wa LBDA alipongeza Kaunti ya Nyamira kwa kutoa huamazisho kuuzu mti ya Bamboo huku akimwomba Gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama kuendelea kuwahamazisha wakulima na kuwatafutaia soko la miti hiyo ili waweze kujiendeleza.
Kwa upande wa ufugaji wa samaki, Atieno aliwaomba wakulima kuanzisha ufugaji wa samaki akiongezea kuwa samaki an afya kwa binadamu.
“Nawaomba wakazi wa Gusii kuanzisha ufugaji wa samaki hata kama kidogo kuna teknologia mpya ya kufuga samaki hao,” alisema Atieno.
Meneja Atieno alisema kuwa wakulima wengi hupuuza mafunzo wanayopewa kuhusu utunzanzaji samaki hoa inayosababisha vifo vya samaki kisha kuwapelekea wafugaji kuacha kufuga samaki. Aliwaomba wakulima hao kuchukua muda wao ili kupata mafunzo hayo kwa makini.
Picha ya aina ya mti wa bamboo. Wakulima kutoka Gisii wameombwa kupanda miti aina ya bamboo kama nja moja ya kutunza mazingira.