Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Walemavu kutoka eneo Bunge la Nyaribari Chache wameiomba Serikali ya Kaunti ya Kisii kuwasaidi kuwachunguza wanaosimamia pesa za walemavu katika eneo hilo kwa madai ya kupora pesa za walemavu zilizotolewa kuwasaidia.

Akiongea siku ya Alhamisi katika eneo la Keumbu kwenye hafla ya kukagua miradi mbali mbali ya maeneo hayo iliyohudhuriwa na Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae pamoja na viongozi wengine, mwenyekiti wa walemavu kutoka eneo hilo John Nyakundi aliiomba Serikali ya kaunti hiyo kuwachunguza wasimaizi wa walemavu kwa madai ya kutowapa pesa zilizotolewa kuwasaidi walemavu.

"Naomba Serikali ya Kaunti ya Kisii kupitia kwa uongozi wa Gavana wetu James Ongwae kuwachunguza baadhi ya wasimamizai wa pesa zetu kwani kuna pesa zilitolewa lakini hatujawahi pokezwa na tunaendelea kusumbuka ilhali tulishatolewa pesa hizo," alihoji Nyakundi.

Kwa mujibu wa Nyakundi, kuna pesa zilitolewa na kaunti hiyo ili walemavu waweze kupokezwa lakini kuna wenye walipora pesa hizo na kuwaacha walemavu wakieendelea kusumbuka na kuangaika.

Aidha, aliiomba Serikali ya Kaunti ya Kisii kuwakumbuka walemavu kila wakati kama njia moja ya kuinua viwango vya maisha yao na kusema kuwa watu wanaotumia pesa za walemavu wanajitakia laana tu wao wenyewe katika familia zao.

Hii si mara ya kwanza visa vya pesa ya walemavu kukosa katika maeneo mbali mbali huku wasimamizi wa pesa hizo wakiombwa kuwajibika na kuwajali walemavu.