Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kaunti ya Kisii imeombwa kuingilia kati na kutatua changamoto wanabiashara wa soko ya Daraja Mbili hupitia wakiendelea na mauzo yao.

Wanabiashara hao wameomba serikali ya kaunti hiyo kuwajengea kivukio cha juu ili kupunguza kujeruhiwa kupitia ajali za barabarani wanapovvuka kutoka ng’ambo moja kuelekea ng’ambo ya pili.

Hii ni baada ya watu wengi kugongwa na magari yanayoleta msongamano mkubwa katika barabara inayopita katikati mwa soko hiyo kila kuchao.

Wakiongea na mwandishi huyu siku ya Alhamisi katika soko hiyo iliyoko katika mji wa Kisii, wanabiashara hao, wakiongozwa na Teresa Kerubo walisema watu hujeruhiwa na magari yanayoendeshwa kwa kasi katika soko hilo, jambo ambalo limewalazimu kuomba serikali ya kaunti kuingilia kati na kuwajengea kivukio hicho wanachohitaji.

“Mimi juma lililopita gari lilinigonga hapa lakini uzuri gari hilo halikuwa linaendeshwa kwa kasi, naomba serikali isikie kilio chetu ili maisha yetu yasiwe hatarini kila wakati na kujenga kivukio hicho,” alihoji Lydiah Bosire, muuza Nyanya katika soko hilo la Daraja.

“Kwa upande wangu huwa ikifika siku ya Alhamisi sifurahii sana maana tunapokuja kwa soko tunaomba Mungu ili siku ikamilike vizuri maana unaeza gongwa na gari wakati wowote kabla ya kufika kwa nyumba,” alidokeza Jastus Osinyo, mwanabiashara wa kuuza begi katika soko hilo.

“Tukijengewa kivukio hicho tutafurahi sana maana itakuwa rahisi kwetu kuvuka kuelekea ng’ambo ingine na tutafanya ubadilishanaji wetu bila taswishi yoyote,” aliongeza Osinyo