Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanakijiji wa Kiamitengi lokesheni ya Gesima wamewaomba wenzao kushirikiana kufungua baadhi ya barabara katika kijiji hicho ili kurahisisha uchukuzi katika eneo hilo.

Wakiongea siku ya Jumanne wakiongozwa na Mzee wa Kijiji Nyakwana Orogo, wakazi hao walisema ukarabati wa baadhi ya barabara katika kijiji hicho zitawanufahisha wafanyibiashara haswa katika sekta ya uchukuzi.

Nyakwana alisema kuwa kuna baadhi ya barabara ambazo zinastahili kufunguliwa katika kijiji hicho ambazo zilifugwa na wakazi ambao nia yao ni kuzuia maendeleo, huku akisema kuwa kabla ya sheria kuchukua mkondo wake, wanastahili kukubali barabara hizo kufunguliwa.

“Kuna barabara ndogo katika kijiji hiki ambazo zinastahili kufunguliwa na sisi wenyenwe ili kujiendeleza kimaendeleo. kwa hivyo, naomba ushirikiano mwema ili kufikia malengo hayo,” alisema Nyakwana.

Aidha, alisema kuwa kinachochangia kuzibwa kwa barabara hizi ni tamaa ya mashamba kati ya wakazi pamoja na fitina vya kijamii, huku akisema kuwa kupitia kwa ofisi ya chifu wa lokesheni hiyo, Magara Makori, wameweka mikakati ya kutatua shida hizo.

“Kwa ushirikiano wa ofisi ya chifu, tumeweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za mashamba zinazochangia kuzibwa kwa barabara hizi na tutahakikisha kuwa kuna uiano wa amani katika kijiji hiki,” aliongezea Nyakwana.

Kwa sasa amewaomba wakazi wote kushirikiana na kukarabati barabara hizo kwa kuwa kijiji hicho huwa na wafanyibiashara wengi wanaotegemea sekta ya uchukuzi.

Kelvin Asiago, mkazi alisema kuwa wamekuwa wakiomba ukarabati wa barabara hizo lakini kwa sasa ana matumain kuwa barabara hizo zitakarabatiwa kwa ushirikiano wa wakazi wa kijiji hicho.