Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa mtaa wa Mwembe Tayari katika mji wa Kisii wamewaomba wanaofanya biashara za kuonyesha filamu kutowaruhusu watoto wadogo kuona filamu hizo.

Wakiongea siku ya Alhamisi katika mtaa huo ulioko katika Wadi ya Kisii ya Kati, eneo Bunge la Nyaribari Chache Kaunti ya Kisii, wakazi hao ambao wengi wao ni wazazi waliwalaumu wafanyibiashara hao kwa kuwaruhusu watoto wadogo wanaostaili kuwa shule kuona filamu hizo huku wakiwaomba kukomesha tabia hiyo.

Kwa mujibu wa wazazi hao, wanao huwaza mambo ya filamu hizo zaidi kuliko masomo na kusema kuwa baadhi ya watoto hutoka nyumba wakidai wanaenda shule ilhali wanaingia katika nyumba hizo za kuonyesha filamu.

Aidha, walisema kuwa viwango vya elimu vimerudi chini kutokana na kuonyeshwa kwa filamu hizo kwa wanafunzi ambao wanafaa kutumia muda wao mwingi kuzitazama filamu hizo, wakiongeza kuwa wengine huiba pesa kutoka kwao za kulipia filamu.

“Tangu kijana wangu aanze kutazama filamu hizo, kiwango chake cha kufanya vyema katika masomo kimerudi chini kwa kuwa haendi shule siku zote kwa ila kutazama filamu,” alihoji mama Salome Kenyambi, mkaazi.

Wakazi hao pia wamewaomba wafantyibiashara hao kuwa hawastaili kuruhusu watato kutazama filamu na kuwaonya kuwa wasipobadilisha kitendo hicho watahakikisha wamechukuliwa hatua ya kisheria.

“Nawaomba wafanyibiashara hawa ambao wanaonyesha filamu katika mtaa huu kutowaruhusu watoto hawa kutizama filamu kwa kuwa huu ni wakati wao wa kusoma ili waweze kujitegemea kimaisha katika siku zijazo,” alihoji James Siringi, mkazi.