Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi wa Wadi ya Gesima eneo bunge la Kitutu Masaba, kaunti ya Nyamira, wamelalamikia kudidimia kwa viwango vya elimu katika wadi hiyo na kuomba washikadau wote katika sekta ya elimu kutafuta njia ya kuinua viwango hivyo.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne katika soko ya Gesima wakaazi hao walisema kuwa viwango vya elimu vimedidimia sana katika eneo hilo na kuomba washikadau wote kushirikiana pamoja na kutafuta mbinu ya kuinua viwango vya elimu juu zaidi.

“Tunahitaji kuwepo kwa umoja katika eneo hili la Gesima haswa kwa sekta ya elimu. Hivi majuzi ndio tulianza kuona elimu ikirudi chini katika shule za upili,”alisema Elijah Okinyi, mkaazi.

Aidha, wakaazi hao walisema wakati huu wa technologia mpya viwango vya elimu vinastahihili kuinuka badala ya kudidimia ili wanafunzi wawe wanapita katika mitihani ya kitaifa.

“Tukiona technologia mpya ikiwawezesha wanafunzi kupita zaidi basi tutafurahia elimu ya kitekinologia kuliko jinsi ilivyokuwa hapo mbeni,” alisema Kepha Makori, mkaazi

Pia wakaazi hao walisema ni jukumu la walimu, wazazi, wanafunzi na wasimamizi wa sekta ya elimu katika wadi hiyo ya Gesima kuungana pamoja na kukubaliana ni lipi watakolifanya kuhakikisha sekta ya elimu imefanya vizuri katika eneo hilo ili kuwakilisha kaunti nzima ya Nyamira.

“Tunatarajia kuona matunda mema ya  mtihani wa mwaka huu katika shule za msingi na za upili. Tumewaomba wasimamizi wote kuwa na ushirikiano ili kuinua elimu na wanafunzi wafurahie matokeo yao,” alisema Jackson Nyambati, mkaazi.