Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa mkuu wa matibabu katika Kaunti ya Nyamira Dkt Jack Magara ametoa ilani kwa wazazi watakaowazulia wanao kupata chanjo ya polio.

Ilani hiyo ilitolewa baada ya Kanisa katoliki kupuuzilia mbali mpango huo wa kuchanja watoto walio chini ya miaka mitano ambao uliafaa kutekelezwa siku ya Jumamosi 1.

Viongozi wa kanisa hilo wanasema kuwa chanjo hiyo inafaa kufanyiwa utafiti wa kutosha. Daktari Magara alisema kwamba kampeini hii itaanza siku ya Jumamosi 1 hadi muda wa wiki mbili na wanalenga kutoa chanjo kwa zaidi ya watoto 100,000 katika kaunti ya Nyamira,alisema haya Alhamisi 30 katika ofisi yake mjini Nyamira. Vilevile aliweza kusema kuwa chanjo hii ni ya muhimu kwa watoto. "Chanjo hii ni yenye manufaa kwa watoto kwani inaweza kuwakinga kutokana na magonjwa sugu ambayo yanaweza kuathiri maisha yao." alisema Magara. Pia aliwasuta wazazi ambao hawatashirikiana na maafisa wa afya katika kipindi hicho. "Ni kinyume kumzuuia mtoto kupata chanjo,ikiwa utapatikana utaweza kukumbana na sheria, naomba ushirikiano." Aliongeza Magara.