Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Viwango vya samaki katika bahari hindi vyaripotiwa kupungua huku kukiwa na tishio la kupanda kwa bei ya samaki.

Akizungumza siku ya Ijumaa, katibu wa vyama vya wavuvi mkoani Pwani, Anuar Abae, alisema upungufu huo umetokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Alisema kuwa maji ya bahari yamekua baridi hali inayopelekea samaki kujificha.

“Hata hivyo, uhaba zaidi unatarajiwa iwapo mvua ya El Nino itanyesha huku wavuvi wengi wakihofia kukumbwa na uhaba wa fedha, sambamba na kukosa mahitaji muhimu hasa ikizingatiwa kuwa uvuvi ndio kitega uchumi kwao,” alisema Abae.

Kwa upande wake, mchuuzi wa samaki, Binti Hassan alisema kuwa anapata wakati mgumu kupata bidha hiyo na kuongeza kuwa hali hiyo imelemaza biashara yake ambayo ndio tegemeo la maisha ya familia yake.