Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanaume wawili wamekamatwa na wakazi na wafanyi kazi wa Kenya Power kwa kunuia kuiba mafuta ya transoma kwa wakidai kuwa wafanyikazi wa Kenya Power.

Wawili hao walikuwa wanajifanya kutengeneza transfoma ya stima kwa kuwa wenyeji walikuwa wamekosa stima kwa siku moja baada ya transoma kupata hitilafu fulani.

Hata hivyo kisa cha kushangaza kilitokea pale wafanyikazi wa Kenya Power walipokuja kutengeneza transfoma hiyo.

Wawili hao walitoroka walipowaona wafanyikazi hao lakini mbio zao ziliambulia patupu pale ambapo wakazi wakiungana na wafanyikazi hao wa Kenya Power waliwanasa na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Kikuyu.

Akidhibitisha kisa hicho siku ya Ijumaa, Mkuu wa polisi katika eneo hilo Mutune Maweu alisema kwamba wawili hao walifikishwa kituoni kwa madai ya kuwa wezi wa mafuta ya transfoma.

Alisema kuwa ulaghai ulikuwa umekiuka na wengi wa wananchi walilaghaiwa pesa zao na watu kama hawa waliojifanya wafanyikazi wa Kenya Power.

Alisema kwamba wawili hao watafikishwa mahakamani na kushtakiwa vilivyo.

Hata hivyo aliwaonya wenye hulka kama hii kwa kusema kwamba siku zao zitawasili na watakamatwa.

"Nawaomba wakazi wawe waangalifu wanapopatana na watu wa aina hii ambao hawana hata sare za kudhibitisha ni wafanyikazi wa kampuni fulani,” alsema Maweu.

Aliwahimiza wawe waangalifu na kuhakikisha kuwa wafanyikazi wa kampuni tofauti wanajitambulisha kabla ya kufanya kazi yoyote.