Vijana kutoka Kaunti ya Kisii wameombwa kutafuta kazi wakati imetangazwa na serikali ya kaunti hiyo licha ya kuwatuma wazazi wao kwa kuwa si wazazi wao wanaomba kazi.
Akiongea siku ya Jumanne katika eneo Bunge la Mugirango Kusini katika hafla ya kukagua miradi katika eneo hilo, David Kombo aliyesimamia tume ya kuwaajiri wafanyikazi katika Kaunti ya Kisii aliwaomba vijana kujitokeza wakati kazi zinapotangazwa ili kuomba nafsi hizo bila kuwatuma wazazi wao kwani wao ndio wanatafuta kazi wala si wazazi wao.
Aidha, Kombo alisema kuwa wajibu wa wazazi ni kuwaelimisha wanao na kumfikisha kiwango cha kutafuta kazi wala sio kuwatafutia kazi.
"Tunapotangaza nafsi za kazi katika Kaunti ya Kisii, wazazi huja kuwatafutia wanao nafsi hiyo licha ya wanao wenyewe kuja kuomba kazi," alihoji Kombo.
Kwa sasa Kombo amewaomba vijana wote kuwajibika na kuwa makini haswa wakati nafasi za kazi zimetangazwa ili wapate kuajiriwa.
"Ni ajabu sana kupata kuwa wakati tunatangaza nafsi za kazi wazazi ndio wanajua kuliko vijana wao, kwa hivyo nawomba vijana wote wa kaunti hii kuwajibika na kuwa macho kila wakati kwani mtafutaji hachoki na akichoka ameshapata," aliongezea Kombo.
Kwingineko alisema kuwa wakati mtu hajafanikiwa katika mkondo wa kwanza isiwe mwisho wake wa kuomba nafasi za kazi kwani kazi ni bahati.