Share news tips with us here at Hivisasa

Wazazi kutoka Kaunti ya Kisii wamependekeza sekta ya elimu iondolewe kutoka serikali ya kitaifa na kuwekwa chini ya serikali za kaunti ili kukomesha migomo inayozuka kila mara.

Wito huo umetolewa baada ya walimu kuingia wiki ya tatu ya mgomo bila kupata nyongeza yao ya mshahara.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu katika mji wa Kisii, mwenyekiti wa wazazi katika kaunti hiyo, Richard Ogembo, alipendekeza serikali ya kitaifa kuacha sekta ya elimu isimamiwe na serikali za kaunti, kwa kudai kuwa serikali kuua imeshindwa kuendesha sekta hiyo kikamilifu.

“Serikali ya kitaifa haina jukumu la kuendelea kushikilia wadhifa wa kusimamamia sekta ya elimu kwani imeshindwa kuendesha sekta hiyo. Naomba sekta hiyo ya elimu iwe nchini ya uongozi wa serikali ya Kaunti ili iwe rahisi kuwalipa walimu,” alisema Ogembo.

“Serikali ikisema haina pesa za kuwalipa walimu ni ishara ya kuonyesha kuwa imeshindwa kuendesha sekta hiyo,” alisema Grace Muma, mzazi.

Wazazi hao walisema idadi kubwa ya watoto wao wanajihusisha na matendo maovu kama vile kushiriki mapenzi, unywaji pombe kwa kutoenda shuleni na kusalia kuzembea nyumbani.