Share news tips with us here at Hivisasa

Wahudumu wa malori ya kubeba mizigo kutoka bandari wamewataka kuongezwa maafisaa wa kushughulikia upakiaji mizigo kuboresha huduma kwa kupunguza misongamano ya malori.

Swala hili linaibuka huku msongamano wa malori ya kupakiwa shehena ukishuhudiwa na ikiwa changamoto kwenye shirika hilo. Wakati mwingi malori hayo huleta mtafaruku katika sekta ya uchukuzi hususan barabara ya kuelekea maeneo ya South Coast kwa sababu ya msongamano wa malori.

Mmoja wa wamiliki wa magari ya uchukuzi ambaye magari yake huondoa mali bandarini, Abdul Shaahliah, kwenye mahojiano siku ya Jumapili amedai kuwa msongamano wa magari eneo hilo utapata suluhu iwapo halmashauri ya bandari ingefanya linalofaa kwa kuongeza mafisaa kuliko kuendelea kutegemea idadi ndogo ambapo kazi huwa nzito kwao.

Moha Abdul anapendekeza kuwe na hata vijana wa vibarua kusaidia shughuli ya kuyaandikisha malori ya kuingia bandarini, na vijana wengine kusaidia katika upakiaji kwa kutumia kreni.

Mwekezaji huyo wa uchukuzi alishangaa ni vipi shirika hilo linaendelea kujidai kuwa lina huduma bora, ilhali malori hulala kwenye bandari hata zaidi ya mwezi yakingoja kuhudumiwa. Alisema sharti mtindo huo ukomeshwe iwapo serikali ya Kenya inataka kuendelea na kuimarisha kiuchumi.

Johnstone Mwangangi, akiwa mmoja wa mwanakamati wa jumuia ya madereva wa malori, aliunga mkono usemi huo akisema madereva wa uchukuzi huathirika pakubwa na hata kusababisha ndoa za wengine kuvunjika kwa kukaa sana na kutokuwa na muda wa kuona familia zao.