Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Kisii imesema kuwa wakazi ambao wana ulemavi wa ngozi wako salama na hakuna kisa hata kimoja kimeripotiwa kwa kudhulumiwa kwa jamii hiyo, na kuwataka watu walio na ulemavu huo kutokuwa na hofu.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne, mkurugenzi wa Idara ya watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti hiyo, Isaac Rogito, alisema kuwa japokuwa kuwa kuna hofu miongoni mwa jamii ya zeruzeru, serikali ya kaunti pamoja na idara yake iko macho.

Alisema kuwa hakuna visa vyovyote ambavyo vimeripotiwa kwenye ofisi yake na kuwataka wahusika kutokuwa na shaka kwa vile idara yake imeweka mikakati ya kuwapa usalama.

Aliitaka jamii na wakazi kwa jumla kutoka kaunti hiyo ya Kisii kutoa ripoti kwenye ofisi yake iwapo wataona yeyote akidhulumiwa na kuwarai wakazi kuwakumbatia zeruzeru na kuachana na kasumba ambayo imekuwa ikisambaa kutoka katika nchi jirani ya Tanzani kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi hufanya mtu kuwa tajiri.

“Si vizuri kuua mtu eti kwasababu kiungo chake kitakufanya uwe tajiri. Hayo ni mashtaka makubwa mbele ya Mungu, na wale ambao wana nia kama hiyo wawe ytayari kuandamwa na sheria,” alisema Rogito.

Aliwata zeruzeru katika kaunti hiyo kuchukua nguo za kuwasitri dhidi ya jua kutoka ofisi yake, ili kuwafaa na kuwakinga dhidi ya kupata maradhi yanahusiana na ngozi kama vile saratani ya ngozi.