Share news tips with us here at Hivisasa

Madereva wawili pamoja na abiria wa matatu zinazobeba abiria katika barabara ya Nakuru-Bahati waliponea kifo leo alfajiri baada ya kuhusika kwenye ajali.

Ajali hiyo ilifanyika karibu na shule ya upili ya wavulana ya Nakuru.

Walioshuhudiwa ajali hiyo wanasema kuwa matatu hizo zilikuwa zikiendeshwa kasi wakati ambapo ajali hiyo ilifanyika. Matatu moja ilikuwa ikitoka Bahati kwenda Nakuru wakati ambapo ziligongana wakati dereva mmoja akijaribu kuipita matatu nyingine.

“Hizi matatu huendeshwa kwa kasi sana, hii ilikuwa inapita hiyo nyingine wakati ambapo ziligongana,” Virgia Maina, aliyekuwa kwenye matatu moja alisema.

Hakuna majeraha wowote walioripotiwa kwenye kisa hicho. Magari hayo yamevutwa na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Central.