Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakulima katika kaunti ndogo ya Kiambu wameombwa kuhudhuria mafunzo ya kilimo Jumamosi katika uwanja wa Ndumberi kwanzia saa nne asubuhi.

Akizungumza katika ofisi yake Ijumaa, afisa wa kilimo Bi Jane Muigai alisema kuwa ofisi ya kilimo imetenga mafunzo maalum kwa wakulima ili kuwawezesha wakulima kuongeza mazao katika ukulima wao.

Alisema kuwa wakulima wengi walikuwa na mashamba makubwa lakini kwa sababu ya kukosa mafunzo hawakuyatumia vizuri ipasavyo. Alisema kuwa mafunzo hayo yatakuwa ya kuwaongezea wakulima maarifa katika sekta ya ukulima ambayo itawaongezea mazao yao shambani.

Afisa huyo pia alitaja kuwa, kutakuwa na mtaalamu wa maswala ya kilimo ambaye atakuwa akiwapa mafunzo wakulima na ambaye pia ana ujuzi wa ukulima na ni mkulima hodari.

Alisema kuwa baadhi ya mafunzo watakayopokea ni; hali ya anga ikilinganishwa na vile vyakula wakulima wanavyopanda, aina ya mchanga ulio katika kaunti hiyo na ni vyakula vipi vinavyoweza kufanya vizuri.

Muigai pia aligusia maswala ya mbolea akisema kuwa wakulima wengi hutumia mbolea ambazo is halali na ndiposa wengi wao huishia kuhesabu hasara katika mazao yao.

"Ninawaomba wakulima waweze kujitokeza kesho katika mafunzo maalum ya kilimo ambayo yatakuwa katika uwanja wa Ndumberi kwanzia saa nne asubuhi mpaka saa adhuhuri," alisema Muiga.