Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja wa umri wa miaka 25 aliuawa siku ya Jumatano kwa kupigwa risisa na maafisi wa polisi kwa hali ya kutatanisha karibu na shule ya kibinafsi ya Dona Olinda, eneo la Mtongwe huko Likoni Kaunti ya Mombasa.

Ndoro Mwema, anayedaiwa kuwa na akili taira, inasemekana alijaribu kuwasumbua maafisa hao wa KDF waliokuwa katika shughuli za kuimarisha usalama, na jamaa huyo akawapiga mawe hali ambayo ilisababisha kupigwa risasi na kuuawa.

Maafisa wa polisi wamethibitisha kuuwawa kwa jamaa huyo na kusema kuwa afisa huyo wa KDF aliyehusika na mauaji hayo kamwe hakukusudia bali alimuua kwa bahati mbaya.

Mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu Mgandi Kalinga ameitaka serikali kuhakikisha kuwa haki dhidi ya mauaji ya mwanamume huyo inapaitikana kwani maafisa hao walimpiga risasi kwa kukusudia.