Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Maafisa wa polisi mjini Mombasa wanalisaka genge la majambazi linalodaiwa kumpiga risasi Afisa mmoja wa polisi na kumuua papo hapo katika kituo cha kukagua magari cha Shika Adabu eneo la Likoni.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, genge hilo la majambazi lililokuwa limeabiri bodaboda na kujihami kwa bunduki linadaiwa kumpiga risasi afisi huyo, kuiba bunduki aina ya G3 na kutoroka.

Akiongea na wanahabari katika la tukio huko Shika Adabu eneo la Likoni mjini Mombasa siku ya Jumanne, Dereva wa lori la kubeba unga la kampuni ya Mombasa Maize Millers Abdullah Azizi alisema kuwa afisa huyo wa polisi alikuwa akitoa ulinzi kwa gari hilo kabla ya kukumbana na maiti yake.

Amesema kuwa afisa huyo alipigwa risasi ya kichwa, tumbo na kifuani kabla ya kuibiwa bunduki aina ya G3 pamoja na shilingi elfu 42 pesa taslimu.

Tayari maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kuwasaka majambazi hao, japo kufikia sasa hakuna jambazi aliyetiwa nguvuni kufuatia kisa hicho.