Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Maskwota zaidi ya 1000 wanaoishi kwenye ardhi inayolengwa kuanzishwa mradi wa nishati ya upepo wamepata afueni baaada ya kuruhusiwa kuishi hapo.

Tume ya Kitaifa ya Ardhi nchini (NLC), kupitia Mwenyekiti wake, Muhammad Swazuri, ilizuru eneo hilo na kuamuru maskwota hao kuendelea kuishi kwenye eneo la mradi hadi pale majadiliano ya kina yatakapotekelezwa kati ya serikali ya kaunti ya Lamu, tume hiyo pamoja na wawekezaji wa mradi huo.

Maskwota hao walikuwa wamepewa makataa ya siku 15 kuhama eneo hilo la mradi na NLC mnamo mwishoni mwa mwezi Januari.

Mradi huo unatarajiwa kutoa takriban megawati 90 za umeme punde utakapokamilika.