Share news tips with us here at Hivisasa

Waziri wa afya katika kaunti ya Kisii Sarah Omache amewashauri akina mama katika kaunti hiyo kujitokeza ili kupimwa ugonjwa wa saratani ya mfuko wa uzazi.

Zoezi hilo litafanyika katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Kisii kwa wiki nzima, zoezi ambalo liling’oa nanga siku ya Jumanne hadi juma lijalo Jumanne ili kuwapima akina mama na kuwatibu bila malipo.

Akizungumza mnamo siku ya Junmanne katika hospitali ya Rufaa ya Kisii wakati zoezi hilo lilikuwa linaanza, Omache aliomba akina mama kutoogopa kupimwa ila kujitokeza kuchunguzwa kimwili ili kupunguza vifo kupitia saratani hiyo ya mfoko wa uzazi.

“Tutakuwa na kambi ya kupima na kutibu saratani ya mfuko wa uzazi kwa akina mama kuanzia leo, Jumanne, kwa wiki nzima,” alisema Omache

“Zoezi hili litachukuwa wiki moja kukamilka na naomba akina mama wa kaunti ya Kisii kujitokeza kwa wingi kwa shughuli hiyo ili kupimwa na kutibiwa,” aliongeza waziri Omache.

Zoezi hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa serikali ya kaunnti ya Kisii kwa ushirikiano na chama cha International Medical Scoop kutoka nchi ya umarekani.

Chama hicho kilitoa usaidizi wa aina hiyo mwaka jana katika kaunti ya Kisii, ambako kiliweza kukabidhi serikali ya Kisii mashine tatu za kupima ugonjwa huo, huku mwaka huu wakiletea serikali hiyo mashine Mbili.