Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama kuu ya Mombasa itatoa hukumu dhidi ya mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la CIPK Sheikh Mohamed Idris, tarehe Machi 24, 2016.

Mshukiwa, Mohamed Soud, anadaiwa kuhusika katika mauaji ya marehemu Sheikh Idris, mnamo Juni 10, 2014, katika eneo la Likoni.

Mwezi Disemba mwaka jana, Soud aliwalaumu maafisa wa usalama kwa kumuhusisha na mauaji hayo pamoja na umiliki wa bunduki na kilipuzi, kwa kujitetea kuwa hana ujuzi wa kutumia silaha hizo hata kidogo.

Mashahidi 17 wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi wao kuhusiana na mauaji hayo.