Vijana kutoka eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini kaunti ya Kisii wamemuomba mbunge wa eneo bunge hilo Jimmy Angwenyi kujitokeza na kuwasilisha ripoti ya hesabu jinsi pesa za hazina ya ustawi maeneo bunge CDf zimetumika kufanya maendeleo kwa mwaka mzima wa 2014/15 katika eneo hilo.
Kulingana na vijana hao, tangu mbunge huyo aingie mamlakani kama mbunge wao hawajafaidika chochote kutoka kwa mbunge wao na kuomba kuelezwa ni maendeleo yapi pesa za CDF zimefanya.
Wakizungmza na waandishi wa habari siku ya Jumatano katika eneo la Mbanda, vijana hao wakiongozwa na mwenyekiti wa vijana katika wadi ya Marani David Omwancha walisema wangependa kuona ripoti ya hesabu ya pesa za mwaka mzima ili kubaini ni maendeleo gani pesa hizo zimekuwa zikifanya.
“Tunaomba mbunge wetu awasilishe ripoti kwetu kama wakazi wa eneo bunge lake ili tujue pesa za CDF zimetumika vipi kufanya maendeleo,”David Omwancha alisema.
“Kile kimetufanya tudai kujua hayo yote ni viile hakuna chochote mbunge huyo amefanya cha maendelo ata kimoja katika eneo bunge letu,” Omwancha alisema.