Utafiti umebainisha kuwa asilimia 55 ya wanafunzi jijini Mopmbasa wana tumia dawa za kulevya.
Kulingana na utafiti uliofanywa na muungano wa sauti ya wanawake hapa Mombasa umekiri kuwepo kwa utumizi wa mihadarati katika shule nyingi za msingi katika kaunti ya Mombasa.
Khadija Wanjiru ,mmoja wa mwanachama wa muungano huo alisema siku ya Jumatano katika eneo la Majengo,kuwa utafiti walioufanywa walipata asilimia 55 ya wanafunzi wanatumia japo bangi, sigara na bugizi.
Khadija amesema tatizo hilo sasa ni kama janga kwa kaunti ya Mombasa na kuitaka serikali ya kaunti kubuni sheria za kudhibiti utumizi wa dawa za kulevya.
Aidha,alitaja maeneo ya Mvita, Kisauni na Bangladesh kama maeneo yaliyoathirika zaidi na jinamizi la dawa za kulevya.
Idadi kubwa ya vijana walio chini ya miaka kumi na nane ambao wengi ni wanafunzi katika shule za upili na msingi wanatumia uraibu wa miraa na bugizi.
Aidha,kulingana na kesi nyingi katika mahakama ya Mombasa zinahusiana na ulanguzi na utumizi wa dawa za kulevya ishara tosha kuwa janga hilo limekita mizizi jijini.