Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya msalaa duniani, Mashirika mbalimbali yasiokuwa ya kiserikali yameungana pamoja kuadhimisha siku hiyo mjini Mombasa.
Akiongea na wanahabari baada ya maadhimisho hayo pamoja na kuifunza jamii jinsi ya kudumisha usafi na mazingira bora ili kujiepusha na maradhi mbalimbali ya kiafya, afisa mkuu wa shirika la Maji na Ufasini eneo la Pwani Bi Hamisa Zajja amesema kwamba jamii inafaa kuzingatia usafi.
Kulingana na Zaja, kutokana na maeneo ya vitongoji duni kukosa vyoo vya kisasa kumechangia pakubwa kuchipuka kwa maradhi ya kiafya, na akasema kwamba mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha kwa jamii inapata elimu bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha vyoo vyao ili kuepukana na maradhi.
Kwa upande wake afisa wa nyanjani katika Shirika la ‘Foundation for sustainable Development’, George Agam amesema kwamba takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 85 ya wanaume hawapendi kuzingatia mazingira bora kwani wengi wao hukosa hata kuosha mikono wanapotoka msalani.
"Asilimia 85 ya wanaume hawanawi mikono wanapotoka msalani na hatua hii basi imechangia kuongezeka kwa maradhi ya kiafya, na siku kama hii ya leo tunawaambia wakazi wazingatie usafi na mazingira bora paomja na kujenga vyoo ili kupunguza maradhi ya kiholela," alisema Agam.
Hata hivyo jamii imehimizwa kushiriki katika vikao vya hamasa ili kufahamu mengi kuhusiana na kudumisha usafi na mazingira bora ili kuendeleza mchakato wa kujenga vyoo mashinani.
Watoto wakinawa mikono baada ya kutoka msalani.Afisa wa nyanjani katika shirika la ‘Foundation for sustainable Development’, George Agam, alisema kwmaba asimilia 85 ya wanaume hawanawi mikono wanapotoka msalani na kuchangia maradhi ya kiafya.