Askari anayedaiwa kuhusika na mauwaji ya askari wengine watatu mwaka wa 2003, katika Kituo cha polisi cha Mtwapa, atafunguliwa mashtaka ya mauwaji katika mahakama kuu ya Mombasa.
Hii ni baada ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa Alexendra Muteti, kuagiza mshukiwa huyo kufunguliwa mashtaka ya mauwaji baadala ya mashtaka ya mauji bila hatia.
Mshtakiwa, Harison Kipng’etich, ameagizwa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kufunguliwa mashtaka ya mauwaji.
Kipng’etich anadaiwa kuwauwa kwa kuwapiga risasi maafisa wenzake Dorine Mwaniki, Alice Kitonye na Jacob Nderi mnamo March 16, 2003 katika Kituo cha polisi cha Mtwapa.
Mshtakiwa atafunguliwa mshataka hayo Februari 22, 2016 baada ya kufanyiwa uchunguzi wa akili.