Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama imefutilia mbali dhamana ya shilingi nusu milioni ya askari anayekabiliwa na mauwaji na kuagiza kuzuiliwa kizimbani hadi kesi itakapotamatika.

Hii ni baada ya askari wa Kituo cha Mtwapa, Harison Lang’at Kiprotich kukosa kuhudhuria vikao vya kesi yake kwa zaidi ya miaka 10 bila sababu zozote.

Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, hakimu Diana Mochache alisema kuwa mshtakiwa amekiuka maagizo ya mahakama na hivyo basi hana budi kusalia rumande.

Aidha, aliongeza kuwa mshitakiwa alihusika pakubwa katika kupoteza faili ya kesi yake mahakamani ambayo ilipatikana hivi majuzi.

Harison Lang’at anadaiwa kuwauuwa kwa kuwapiga risasi maafisa wenzake, Jacob Nderi, Dorine Wawira na Alice Kitonye wote kutoka kituo cha Mtwapa mnamo Machi 16, 2003.

Kesi yake itasikilizwa Disemba 24, 2015.