Askari wawili wa serikali ya kaunti ya Mombasa, wanauguza majeraha baada ya kugongwa na matatu iliyokaidi amri ya kusimama katika eneo la Bombolulu.
Akithibitisha kisa hicho siku ya Jumanne, afisa mkuu wa kitengo cha askari wa kaunti, Charles Changawa, alisema kuwa dereva wa matatu hiyo iliokuwa ikitoka mtwapa alikaidi amri ya askari hao ya kusimama kwa kosa la kuendesha gari upande usiokuwa wake.
Aidha aliongeza kuwa dereva wa matatu hiyo aliigeuza na kurudi kisha akasimamisha na kuanza kurushia mawe gari la kaunti lililokuwa likiwafauta wakiwa na baadhi ya manamba eneo la Bombolulu jambo lililopelekea kuvunjwa kwa kioo cha gari hilo na kisha jamaa hao kutoweka.
Kisa hicho kimeripotiwa katika kituo cha polisi cha Bamburi na tayari msako umeanzishwa kuwatambua jamaa waliotekeleza uhalifu huo.