Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki katika Jimbo la Mombasa Martin Musonde amezindua rasmi msafara wa kueneza ujumbe wa amani mjini Mombasa na maeneo mengine katika kaunti ya Mombasa.

Katika mkao na wanahaabri katika Kanisa Katoliki la Holy Ghost Cathedral mjini Mombasa, Askofu Kivuva amesema kwamba msafara huo unatarajiwa kuwaunganisha wakazi wa Pwani pamoja na kuenea ujumbe wa amani na kuondoa chuki miongozi mwa wakazi.

Kulingana na Askofu Kivuva, msafara huo wa vijana wa kikiristu umepangwa kuelekea jijini Nairobi kuanzia hapo kesho na kufanyika kwa maombi ya pamoja katika maeneo ya Macknon road, Voi na Machakos kabla ya kuwasili jijini Nairobi kuhudhuria ibada maalum itakayoongozwa na Papa Francis.

Askofu Kivuva aliongeza kwamba tayari zaidi ya vijana 900 na wakazi 2,000 kutoka jimbo la Mombasa linalojimuisha kaunti ya Mombasa, Kwale, Kilifi na Taita Taveta wanatayarijiwa kuhudhuria ibada hiyo maalum jijini Nairobi, huku akiwahakikishia waumini usalama dhabiti.

Amewataka wakazi wa eneo la pwani kutobaguana kwa misingi ya kidini, kikabila au kisiasa, na badala yake kuchukua hatua ya kuungana pamoja kwani ujumbe wa Baba Mtakatifu Papa Francis unaunganisha jamii ya Kenya na bara la Afrika pamoja.

"Tunawaomba wakazi wa eneo la pwani na Mombasa kuungana pamoja na kueneza ujumbe wa amani ili kuleta pamoja Wakenya na kuondoa ubaguzi wa kidini, kikabila na kisiasa, na badala yake kuchukua mfano wa unyenyekezi wa Baba Mtakatifu na kueneza amani," alisema Kivuva.

Tayari idara ya usalama kaunti ya Mombasa imeahidi kuimarisha usalama kwa msafara huo, huku ikitoa onyo kali kwa wanaopanga kuvuruga msafara huo kuwa watakabiliwa kikamilifu na maafisa wa usalama.