Mbunge wa Nyali Hezron Awiti ameahidi kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita unyakuzi wa ardhi katika eneo bunge lake.
Akizumgumza Jumanne katika mtaa wa Matopeni eneo la Kongowea, Awiti aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa atafanya juhudi zote katika kukabiliana na tatizo hilo ili wakazi waishi kwa amani na utulivu.
Awiti amesisitiza kuwa atajitahidi kuwatetea wakazi hao bungeni ama hata mahakani ili haki na usawa upatikane kwa wanaohangaishwa kwa sababu ya ardhi.
Aidha, amependekeza hatua ya raisi Kenyatta ya kutoa hakikisho kuwa eneo hilo la Matopeni kuwa litabaki kuwa miliki ya wakazi wa eneo hilo wala si mabwenyenye wanaodai kumiliki ardhi hiyo.