Bawabu mmoja aliyekua akihudumu kwenye kituo cha petroli cha Top Ten huko Langa Langa Jumapili jioni alitiwa mbaroni baada ya kupatikana akiiba. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Bawabu huyo alipatikana na wenzake alipokua akijaribu kupitisha lita arobaini za mafuta ya diseli. 

Mabawabu wenzake walimnasa na kumsalimisha kwa meneja wa kituo hicho bwana Joseph Mwangi, ambaye aliwafahamisha maafisa wa usalama waliomtia mbaroni na kumpeleka katika kituo kikuu cha polisi mjini. 

Inasemekana bawawabu huyo alikua na mazoea ya kuiba, na wenzake walikua wamemwekea mtego ili kumnasa. 

Bawana Mwangi alisema wamekua wakipoteza vitu vingi kazini, ndiposa wakaamua kuweka mtego uliomnasa bawambu huyo.

"Tumekua tukipoteza vitu hapa na tukapata fununu kuwa huyu ndiye aliyekua akituhangaisha, ndiposa nikaongea na hawa wenzake tukaweka mtego uliomnasa," alisema Mwangi.

Kwa sasa bawabu huyo yumo katika korokoro ya polisi akitegea kufikishwa mahakamani siku ya Jumanne.