Uhaba mkubwa wa viazi unashuhudiwa mjini Nakuru huku mvua ikiendelea kunyesha katika maeneo mengi ya kaunti.
Kulingana na utafiti uliofanywa na mwandishi huyu,mengi ya masoko yanakos bidhaa hii ambayo kwa hutegemewa pakubwa na familia nyingi za mijini.
Katika soko kuu la Nakuru ndoo moja iliyokuwa ikiuzwa kwa shilingi mia mbili hamsini sasa inauzwa kwa shilingi mia nne kutokana na ukosefu huo
Baadhi ya wafanyibiashara wameelea kuwa uhaba huo unatokana na mvua kubwa zinazonyesha katika maeneo yanayokuza bidhaa hiyo.
Grace Nyambura ambaye ni muuzaji jumla wa viazi mjini Nakuru amesema kuwa wamelazimika kupandisha bei kutoka na ukosefu wa viazi.
“Wakati mvua ilianza kunyesha,viazi navyo vikapotea kwa sababu wakulima hawawezi kuvuna viazi kukiwa na mvua kubwa na hii imepelekea kupanda kwa bei katika masoko,” alisema Nyambura.
Timothy Njogu ambaye ni mkulima muuzaji wa viazi alisema kuwa huenda bei ikapanda zaidi mwezi desemba iwapo mvua itaendelea kunyesha.
“Kama mvua haitapungua basi tutazidi kuona bei ikipanda haswa mwezi wa disemba ambao una sherehe nyingi sana,” alisema Njogu.