Vijana wamehimizwa kutojihusisha na matendo yatakayopelekea kuambukizwa ugonjwa wa ukimwi.
Akizungumza katika uwanja wa Nyamaiya siku ya jumatano wakati wa uzinduzi wa kliniki cha kutembezwa za Beyond Zero, katika kaunti ya Nyamira, mkewe rais Margaret Kenyatta aliwashauri vijana kujiepusha na matendo ambayo yatawaletea ugonjwa huo.
Kulingana na Kenyatta, vijana ndio viongozi wa kesho na kuna haja ya kila kijana kujilinda ili kutopatwa na hatari ya ugonjwa wa ukimwi ili kujiendeleza kimaisha yasio na athari za ukimwi.
“Naomba vijana wote msiwe mnafanya matendo yale yatapelekea nynyi kuambukiza ugonjwa wa ukimwi kwani nyinyi ndo viongozi wa kesho na kuna haja ya kila kijana kujilinda ili kuuepuka,” alisema Bi Kenyatta.
Aidha, mama huyo wa taifa aliwashauri wananchi kutowatenga watu walioathirika na ugonjwa huo katika jamii.
“Naomba msiwatenge wanaoishi na ugonjwa wa ukimwi kwani ni binadamu wa kawaida, tofauti ni ile wako na ugonjwa wa ukimwi ambapo kwa mara nyingi walipata viruzi hivyo kwa kutopenda ,” aliongeza Bi Kenyatta.
Hata hivyo, mkewe Rais alizindua rasmi kliniki ya Beyond Zero katika kaunti hiyo huku akiwashauri akina mama kujifungilia hospitalini na kwa mara nyingine kutumia kliniki hiyo.
Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama aliyekuwa ameeandamana na mkewe Naomi walimpongeza mama wa taifa kwa mchango huo.