Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Kitutu Masaba Timothy Bosire amepongezwa kwa kuanzisha kukarabati barabara ya kutoka eneo la Metemaywa-Kebirigo.

Hii ni baada ya barabara hiyo kuonekana kuwa mbovu kwa muda mrefu na kusimamisha shughuli za uchukuzi kila wakati mvua inaponyesha na kupelekea wengi kupata hasara.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatatu katika eneo la Metamaywa, wakazi wa eneo bunge hilo walimpongeza Bosire kwa juhudi za kuanzisha kukarabati barabara hiyo kwa kuweka lami ili kurahisisha shughuli za uchukuzi.

“Barabara hii imekuwa mbovu kwa muda mrefu na kusababisha kutopitika haswa inaponyesha, wabunge wengine waliokuwa katika nyadhifa za uongozi wameondoka bila kukarabati barabara hii,” alihoji Okindio.

“Mbunge wetu Bosire ameanza kukarabati barabara hii na tunampongeza kwa maenedeleo hayo na akarabati barabara zingine za eneo bunge hili ili sekta ya uchukuzi iweze kuimarikia zaidi hapa Kitutu Masaba,” alisema David Moikoyo mkazi mmoja.

Kwa majuma matatu yaliyopita, mbunge huyo alitangaza kushirikiana na shirika la KeRRA kukarabati barabara za eneo bunge lake ili kuhakikisha ahadi alizotoa amezitimiza kabla ya uchaguzi ujao.

Pia wakazi waliomba Bosire kushirikina na gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama kuleta maendeleo mengi katika eneo bunge hilo kwani lao ni kuona maendeleo yakija karibu nao na kufurahia uongozi wa sasa.