Mfanyibiashara katika kaunti ya Mombasa Ali Mboga amedai kuunga mkono mswada uliyoko bungeni kuhusu wangombea wa eneo bunge nchini kuwa na viwango vya elimu vya shahada ya degree.
Kulingana na Mboga kufuatia kwa wananchi kuwachagua viongozi waliyo na viwango vya chini kielimu kumepelekea kukosa maswala muhimu ya kimaendeleo.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Mboga ambaye pia ametangaza kugombea ubunge wa Kisauni katika uchaguzi mkuu ujao, amesema kuwa ili kuwatekelezea wakenya maendeleo ni lazima kubadilisha uongozi uliyopo.
“Tunalihimiza bunge la kitaifa kupitisha ule mswada uliyoko bungeni kwa sasa kuwa mbunge wa kitaifa lazima awe na shahada ya digirii kabla ya kuwania kiti hicho ili kubadilisha uongozi wa nchi”,alisema Mboga.
Amesema kuwa makosa makubwa wakazi wa kaunti ya Mombasa waliyotekeleza wakati wa uchaguzi uliyopita ni kuwachagua viongozi wasio na maono kutokana na kuwa na viwango vya chini kielimu.
Mfanyibiashara huyo katika kaunti ya Mombasa amahidi kutekeleza maendeleo katika eneo bunge hilo sasa na hata baada ya wakazi kumchagua katika uchuguzi mkuu ujao mwaka 2017.