Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Molo Jacob Macharia amesema kuwa elimu ni nguzo muhimu katika jamii yoyote ile na kuna haja ya viongozi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inafadhiliwa vilivyo.

Akiongea katika shule ya upili ya Kibunja, eneo bunge lake, siku ya Jumanne, Macharia alisema kuwa atahakikisha kuwa fedha za maendeleo ya maeneo bunge CDF zimetumika kuinua sekta ya elimu.

Macharia alikuwa katika shughuli ya kukagua ukarabati wa madarasa kwenye shule hiyo uliofadhiliwa na CDF.

“Shule hii sasa imekuwa afueni kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakilazimika kutembea safari ndefu hadi mjini Molo,” Macharia alisema.

Shule hiyo inatarajiwa kuanza kuwasajili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuanzia Februari. Macharia amesema shule hiyo pia itatoa nafasi za kazi kwa wakazi ambao wako kwenye taaluma ya ualimu kwani wanahitaji waalimu.