Share news tips with us here at Hivisasa

Muungano wa wabunge waliyouasi mrengo wa Cord, sasa wanasema kuwa mshindi kwenye uchaguzi mdogo wa Malindi uliyofanyika siku ya Jumatatu alikuwa Philip Charo wa Jubilee.

Kwenye taarifa iliyotumwa kwa wanahabari baada ya mkao wa mazungumzo wa viongozi wa chama hicho mjini Malindi siku ya Ijumaa, mwenyekiti wa wabunge wa Pwani Gideon Mung’aro alisema kuwa viongozi hao watatoa taarifa zaidi kuhusiana na uchaguzi huo siku ya Jumanne.

Mung’aro alisema kuwa viongozi hao wako na ushahidi wa kutosha kuhusu yale yaliyotokea kwenye uchaguzi huo na kwamba kwa sasa wanaachia swala hilo kwa maafisa wa upelelezi ili kubaini ukweli halisi.

“Tunaushahidi wakutosha kuhusu jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa na tutatoa taarifa yetu siku ya Jumanne baada ya uchunguzi wa maafisa wa upelelezi kukamilika,” alisema Mung’aro.

Kwa upande wake mbunge wa Kilifi Kusini Mustafa Iddi amepuzilia mbali hatua ya Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho kushinikiza kutimuliwa kwa wabunge waasi kutoka kwa muungano wa Cord na akamtaka kukoma mara moja kwani wao walichaguliwa na wananchi.

“Tunamtaka Gavana Joho kukoma kuingilia hata kama yeye ni Naibu Kinara wa chama cha ODM sisi tulichaguliwa na wananchi na iwapo tunahitaji kukihama chama cha ODM tutakihama hakuna mtu anawezakutuzuilia katiba iko wazi na siasa ni demokrasia,” alisema Mustafa.