Chama cha Kenya National Congress [KNC} kitafungua ofisi zake katika kaunti za Kisii na Nyamira ili kutoa huduma bora kwa jamii ya mkisii kisiasa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na wanachama wa chama hicho, lengo la kufungua ofisi zake katika kaunti hizo ni kuwaleta jamii ya mkisii pamoja kisiasa kwani chama hicho kilianzishwa na George Anyona na kuna haja ya chama hicho kuendelea na kutumiwa na wanasiasa kuwania viti mbalimbali vya kisiasa.

Akizungumza siku ya Jumanne katika mkahawa mmoja mjini Kisii, mwenyekiti wa chama hicho Atati Kengere aliomba wanasiasa wa kaunti za Kisii na Nyamira kuungana pamoja na kutumia KNC ili kutafuta uongozi kupitia chama hicho.

“Chama cha KNC ni chama chetu wakisii , naomba viongozi wote tujiunge pamoja tuendeleze chama chetu na tukitumie chama hiki kutafuta uongozi katika nyadhifa mbalimbali,” alisema Atati Kengere.

Aidha, Kengere aliomba vijana na akina mama kujitokeza kwa wingi na kujiunga na chama hicho ili kuinua chama hicho kwa njia ya kisiasa.