Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa ODM Nakuru Dennis Okomol ametoa wito kwa idara ya mahakama kujisafisha kutokana na shtuma za ufisadi.

Matamshi ya Okomol yanajiri wakati mbunge wa Mbita Millie Odhiambo akidai kwamba iwapo Jaji Phillip Tunoi atapatikana na hatia katika shtuma za ufisadi dhidi yake basi huenda kuna uwezekano uamuzi kuhusu uchaguzi wa urais haukuwa huru na wa haki.

 Mbunge huyo wa Mbita anasema kuwa jaji Tunoi alikuwa miongoni mwa wale waliotoa uamuzi kuhusiana na kesi ya uchaguzi mkuu 2013. 

Ameongeza kuwa iwapo ufisadi utakithiri katika idara ya mahakama basi hakutakuwa na pengine pa kukumbilia.