Mwenyekiti wa chama cha wazazi nchini tawi la Nyamira Vincent Mbura amejitokeza kuwaonya vikali walimu wakuu wa za umma dhidi ya kuongeza karo bila ya kuwashauri washikadao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubia wanahabari mjini Nyamira, Mbura alisema kwamba wizara ya elimu nchini inastahili kufanya uchunguzi wa kubaini shule ambazo bado zimekaidi amri ya kutorudisha chini karo ili walimu wakuu husika wachukuliwe hatua kali za kisheria.

“Tunaishkuru wizara ya elimu nchini kwa hatua ya kupunguza viwango vya karo ya shule vinavyostahili kulipwa na linalostahili kwa sasa ni kuhakikisha kwamba walimu wakuu wa shule wanazingatia hilo ili wazazi wasiendelee kunyanyaswa,” alisema Mbura.

Mbura aidha aliongeza kwa kuwahimiza wazazi kote nchini kuwaripoti walimu wakuu wa shule wanaokiuka agizo la katibu wa wizara ya elimu ili kuhakikisha mianya ya ufisadi inazibwa.

“Ni himizo langu kwa wazazi kote nchini kuchukua hatua ya kuwaripoti walimu wakuu wa shule wanaokiuka agizo la wizara ya elimu dhidi ya viwango vya karo vinavyostahili kulipwa,” aliongezea Mbura.