Mkuu wa eneo la Bonde la Ufa kusini Wanyama Musiambo ametangaza kuwa chifu mmoja katika eneo la Njoro amesimamishwa kazi kwa muda kufuatia madai kwamba alikuwa anachochea jamii moja kushambulia nyingine kwenye shamba tata la Ngongongeri.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea kwenye shamba hilo ambalo limeshuhudia machafuko za kikabila  tangia siku ya Jumatatu, Musiambo aliongeza kwamba chifu huyo ni miongoni mwa wale wataofikishwa mahakamani kujibu madai ya uchochezi mnamo Mechi 11.

Aidha aliongeza kuwa maafisa wa polisi wataendelea kushika doria kwenye mipaka ya kaunti ndogo za  Molo na Njoro ambazo zimeathirika na machafuko hizo na pia kujaribu kuwakamata wale ambao walikuwa wananchochea wakaazi huku taharuki ikizidi kutanda.

Tayari zaidi ya nyumba kumi zimeripotiwa kuchomwa kwa kile wakaazi wanadai kuwa ni mashambulizi yaliyochochewa na mwanasiasa mstaafu katika eneo hilo.